×

Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa 60:4 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Mumtahanah ⮕ (60:4) ayat 4 in Swahili

60:4 Surah Al-Mumtahanah ayat 4 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Mumtahanah ayat 4 - المُمتَحنَة - Page - Juz 28

﴿قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ ﴾
[المُمتَحنَة: 4]

Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قد كانت لكم أسوة حسنة في إبراهيم والذين معه إذ قالوا لقومهم, باللغة السواحيلية

﴿قد كانت لكم أسوة حسنة في إبراهيم والذين معه إذ قالوا لقومهم﴾ [المُمتَحنَة: 4]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwa hakika mlikuwa na kiigizo kizuri, enyi Waumini, kwa Ibrāhīm na wale waliokuwa pamoja na yeye waliposema kuwaambia wakanushaji Mwenyezi Mungu, «Sisi tumejiepusha na nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tumewakanusha nyinyi na tumeukataa ukafiri mlionao, na umejitokeza nje uadui na machukivu ya milele baina yetu sisi na nyinyi madamu bado mko kwenye ukanushaji wenu, mpaka mmuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake.» Lakini haliingii kwenye kuigiza tendo la Ibrāhīm la kumuombea msamaha babake, kwa kuwa hilo lilitokea kabla ya Ibrāhīm kufunukiwa kuwa babake ni adui wa Mwenyezi Mungu, na alipofunukiwa kuwa yeye ni adui wa Mwenyezi Mungu alijiepusha na yeye. Mola wetu! Kwako wewe tumetegemea, na kwako wewe tumerejea kwa kutubia, na kwako wewe ndiko marejeo Siku ya Kiyama
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek