Quran with Swahili translation - Surah Al-Mumtahanah ayat 5 - المُمتَحنَة - Page - Juz 28
﴿رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ﴾
[المُمتَحنَة: 5]
﴿ربنا لا تجعلنا فتنة للذين كفروا واغفر لنا ربنا إنك أنت العزيز﴾ [المُمتَحنَة: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wa wale waliokukanusha wewe, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo na hapo waseme, «Lau hawa wangalikuwa kwenye haki haingaliwapata adhabu hii,» na wazidi ukafiri. Na utufinikie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake |