Quran with Swahili translation - Surah At-Taghabun ayat 17 - التغَابُن - Page - Juz 28
﴿إِن تُقۡرِضُواْ ٱللَّهَ قَرۡضًا حَسَنٗا يُضَٰعِفۡهُ لَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ ﴾
[التغَابُن: 17]
﴿إن تقرضوا الله قرضا حسنا يضاعفه لكم ويغفر لكم والله شكور حليم﴾ [التغَابُن: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Iwapo mtatoa mali yenu katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Yeye na kwa moyo mzuri, Atawaongezea Mwenyezi Mungu thawabu za ambacho mmekitoa na Atawasamehe madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kurudisha shukrani kwa watoaji kwa kuwapa malipo mema ya kile walichokitoa, ni Mpole kwa kutoharakisha mateso kwa wanaomuasi |