Quran with Swahili translation - Surah AT-Talaq ayat 1 - الطَّلَاق - Page - Juz 28
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحۡصُواْ ٱلۡعِدَّةَۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ رَبَّكُمۡۖ لَا تُخۡرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخۡرُجۡنَ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ لَا تَدۡرِي لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحۡدِثُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ أَمۡرٗا ﴾
[الطَّلَاق: 1]
﴿ياأيها النبي إذا طلقتم النساء فطلقوهن لعدتهن وأحصوا العدة واتقوا الله ربكم﴾ [الطَّلَاق: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ewe Mtume! Pindi mnapotaka, wewe na Waumini, kuwapa talaka wake zenu, basi wapeni talaka wakiwa kwenye hali ya kukabili kipindi cha wao kukaa eda- yaani kwenye hali ya usafi ambao hakukupatikana kuingiliwa, au katika hali ya mimba iliyo wazi- na mshike hesabu ya eda, mpate kujua muda wa kuwarejea iwapo mtataka kuwarejea, na muogopeni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Wala msiwatoe wanawake waliopewa talaka kwenye majumba wanayokaa mpaka eda lao limalizike, nalo ni hedhi tatu kwa asiyekuwa mdogo (asiyeingia damuni) na si kwa aliyekata tamaa ya kuingia damuni (kwa uzee) wala mwenye mimba. Na haifai kwa wanawake hao kutoka majumbani mwao wao wenyewe isipokuwa watakapofanya kitendo kiovu cha waziwazi kama vile uzinifu. Na hizo ndizo hukumu za Mwenyezi Mungu alizozipitisha kwa waja Wake. Na Mwenye kuzikiuka hukumu za Mwenyezi Mungu, basi huyo amejidhulimu nafsi yake na ameipeleka mahali pa maangamivu. Hujui, ewe mtoaji talaka, kwamba Mwenyezi Mungu huenda, baada ya talaka hiyo, Akaleta jambo usilolitazamia ukaja ukamrudia |