Quran with Swahili translation - Surah At-Tahrim ayat 6 - التَّحرِيم - Page - Juz 28
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ قُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَأَهۡلِيكُمۡ نَارٗا وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلۡحِجَارَةُ عَلَيۡهَا مَلَٰٓئِكَةٌ غِلَاظٞ شِدَادٞ لَّا يَعۡصُونَ ٱللَّهَ مَآ أَمَرَهُمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ ﴾
[التَّحرِيم: 6]
﴿ياأيها الذين آمنوا قوا أنفسكم وأهليكم نارا وقودها الناس والحجارة عليها ملائكة﴾ [التَّحرِيم: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Zilindeni nafsi zenu kwa kuyatenda yale ambayo Amewaamrisha kwayo Mwenyezi Mungu na kuyaepuka yale ambayo Amewakataza nayo, na walindeni watu wenu kwa kile mnachotumia kujilinda nyinyi wenyewe na Moto ambao kuni zake ni watu na majiwe. Watasimamia kuadhibiwa watu wa Motoni Malaika wenye nguvu walio thabiti katika usimamizi wao, wasioenda kinyume na Mwenyezi Mungu katika maamrisho Yake na wanaotekeleza yale wanayoamrishwa |