Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 12 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ ﴾
[الأعرَاف: 12]
﴿قال ما منعك ألا تسجد إذ أمرتك قال أنا خير منه خلقتني﴾ [الأعرَاف: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema hali ya kumkemea Iblisi kwa kuacha kwake kumsujudia Ādam, «Ni lipi lililokuzuia usisujudu nilipokuamuru?» Iblisi akasema, «Mimi ni bora kuliko yeye, kwa kuwa mimi nimeumbwa kwa moto na yeye ameumbwa kwa udongo.» Akaona kuwa moto ni bora kuliko udongo |