Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 137 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُۥ وَمَا كَانُواْ يَعۡرِشُونَ ﴾
[الأعرَاف: 137]
﴿وأورثنا القوم الذين كانوا يستضعفون مشارق الأرض ومغاربها التي باركنا فيها وتمت﴾ [الأعرَاف: 137]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tukawarithisha Wana wa Isrāīl, waliokuwa wakifanywa wanyonge, pande za mashariki na magharibi ya ardhi, nazo ni sehemu za miji ya Sham, tulizozitia baraka kwa kutoa mazao na matunda na mito. Na limetimia neno jema la Mola wako, ewe Muhammad, kwa Wana wa Isrāīl kwa kuwapa utulivu katika ardhi kwa sababu ya kuvumilia kwao makero ya Fir'awn na watu wake. Na tukayavunjavunja yale maamirisho na mashamba ambayo Fir'awn na watu wake walikuwa wakiyatengeneza, na majengo na majumba na mengineyo waliokuwa wakiyajenga |