Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 149 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ ﴾
[الأعرَاف: 149]
﴿ولما سقط في أيديهم ورأوا أنهم قد ضلوا قالوا لئن لم يرحمنا﴾ [الأعرَاف: 149]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na walipojuta wale walioabudu kigombe badala ya Mwenyezi Mungu pale aliporudi Mūsā kwao, na wakaona kwamba walipotea njia ya sawa, na waliondoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, walianza kuukubali uja na kuomba kufutiwa makosa yao wakasema, «Mola wetu Asipoturehemu kwa kukubali toba yetu, na kufinika kwayo madhambi yetu, tutakuwa ni wenye kuangamia ambao matendo yao mema yamepita bure.» |