×

Na alipo rudi Musa kwa watu wake, naye amekasirika na kuhuzunika, alisema: 7:150 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:150) ayat 150 in Swahili

7:150 Surah Al-A‘raf ayat 150 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 150 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[الأعرَاف: 150]

Na alipo rudi Musa kwa watu wake, naye amekasirika na kuhuzunika, alisema: Ni maovu yalioje mlio nifanyia nyuma yangu! Je, mmeitangulia amri ya Mola wenu Mlezi? Na akaziweka chini zile mbao, na akamkamata kichwa ndugu yake akimvutia kwake. (Haarun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika hawa watu wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa. Basi usiwafurahishe maadui juu yangu, wala usinifanye pamoja na watu madhaalimu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولما رجع موسى إلى قومه غضبان أسفا قال بئسما خلفتموني من بعدي, باللغة السواحيلية

﴿ولما رجع موسى إلى قومه غضبان أسفا قال بئسما خلفتموني من بعدي﴾ [الأعرَاف: 150]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Aliporejea Mūsā kwa watu wake akiwa na hasira na huzuni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimpa habari kwamba watu wake wamepatikana na mtihani na kwamba Sāmirīy amewapoteza. Mūsā alisema, «Ni ubaya ulioje mlioufanya nyuma yangu baada ya mimi kuondoka! Je mumeitangulia amri ya Mola wenu?» Yaani, mulikufanyia haraka kuja kwangu kwenu, na hali ni jambo lililopangwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?. Mūsā alizitupa mbao za Taurati kwa kuwakasirikia watu wake walioabudu kigombe na kwa kumkasirikia ndugu yake Hārūn. Akakishika kichwa cha Hārūn na akakivuta upande wake. Hārūn alisema kwa kubembeleza, «Ewe mwana wa mamangu, ‘Hakika hawa watu walinidharau, waliniona ni mnyonge na walikaribia kuniua, kwa hivyo usiwafurahishe maadui kwa unayonifanya na usiniingize katika hasira zako ukanifanya ni pamoja na wale walioenda kinyume na amri yako na wakaabudu kigombe.’»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek