Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 205 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِي نَفۡسِكَ تَضَرُّعٗا وَخِيفَةٗ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ ﴾
[الأعرَاف: 205]
﴿واذكر ربك في نفسك تضرعا وخيفة ودون الجهر من القول بالغدو والآصال﴾ [الأعرَاف: 205]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mtaje Mola wako, ewe Mtume, ndani ya nafsi yako kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumdhalilikia, hali ya kumcha Yeye moyoni, na umuombe kwa namna ya kati na kati baina ya kutoa sauti na kuifanya chini, katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, na usiwe ni miongoni mwa wenye kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu na kupumbaa katika nyakati zao zinginezo |