Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 35 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأۡتِيَنَّكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ ﴾
[الأعرَاف: 35]
﴿يابني آدم إما يأتينكم رسل منكم يقصون عليكم آياتي فمن اتقى وأصلح﴾ [الأعرَاف: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi wanadamu! Pindi watakapokuja kwenu Mitume wangu, miongoni mwa watu wenu, wakiwasomea aya za Kitabu changu na kuwafahamisha hoja juu ya ukweli wa yale waliyokuja nayo, basi watiini, kwani mwenye kujikinga na hasira zangu na akayatengeneza matendo yake, hao hawatakuwa na hofu na mateso ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama wala hawatahuzunika juu yale yaliyowapita miongoni mwa hadhi za duniani |