Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 48 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٗا يَعۡرِفُونَهُم بِسِيمَىٰهُمۡ قَالُواْ مَآ أَغۡنَىٰ عَنكُمۡ جَمۡعُكُمۡ وَمَا كُنتُمۡ تَسۡتَكۡبِرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 48]
﴿ونادى أصحاب الأعراف رجالا يعرفونهم بسيماهم قالوا ما أغنى عنكم جمعكم وما﴾ [الأعرَاف: 48]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na watu walioko Al-A’rāf watawaita wanaume, miongoni mwa viongozi wa makafiri waliomo motoni, wanaowajua kwa alama zao fulani zinazowatenganisha wawaambie, «Hayakuwafaa chochote mali mliokuwa mkiyakusanya ulimwenguni wala watu; pia hakikuwafaa kiburi chenu kilichowafanya nyinyi msimuamini Mwenyezi Mungu na msiikubali haki.» |