Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 65 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿۞ وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴾
[الأعرَاف: 65]
﴿وإلى عاد أخاهم هودا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله﴾ [الأعرَاف: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tulimtuma, kwenda kwa watu wa kabila la 'Ād, ndugu yao Hūd, walipoabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, akawaambia, «Muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwaYeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada. Je, hamuiogopi adhabu ya Mwenyezi Mungu na hasira Zake kwenu?» |