Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 71 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿قَالَ قَدۡ وَقَعَ عَلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ رِجۡسٞ وَغَضَبٌۖ أَتُجَٰدِلُونَنِي فِيٓ أَسۡمَآءٖ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّا نَزَّلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٖۚ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ ﴾
[الأعرَاف: 71]
﴿قال قد وقع عليكم من ربكم رجس وغضب أتجادلونني في أسماء سميتموها﴾ [الأعرَاف: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hūd alisema kuwaambia watu wake, «Mshashukiwa na adhabu na ghadhabu kutoka kwa Mola wenu, Aliyetukuka na kuwa juu, «Mwajadiliana na mimi juu ya masanamu hawa mliowaita waungu, nyinyi na mababa zenu? Mwenyezi Mungu Hakuteremsha hoja yoyote wala dalili ya kuwa waabudiwe, kwani wao wameumbwa, Hawadhuru wala hawanufaishi; mwenye kuabudiwa peke yake si mwengine ni Muumba, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Basi ngojeni kuteremkiwa na adhabu, kwani mimi, pamoja na nyinyi, nangojea kuteremka kwake. Huu ni upeo wa kuonya na kutisha.» |