Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 95 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 95]
﴿ثم بدلنا مكان السيئة الحسنة حتى عفوا وقالوا قد مس آباءنا الضراء﴾ [الأعرَاف: 95]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha tukaigeuza hali nzuri ya mwanzo mahali pa hali mbaya, wakawa wana afya katika miili yao, na ukunjufu na neema katika mali zao, ili kuwapa muhula, kwani wakashukuru. Hayo yote hayakuwa na faida kwao, na hawakuzingatia wala hawakukomeka na ushirikina waliokuwa nao na wakasema, «Hii ndiyo hali ya ulimwengu kwa watu wake, kuna siku njema na siku mbaya; na hayo ndiyo yaliyowapitia baba zetu hapo nyuma.» Basi, punde si punde, tuliwashika kwa adhabu wakiwa wametulia, hawakuwa wakifikiria kuwa wataangamizwa |