Quran with Swahili translation - Surah Al-Jinn ayat 18 - الجِن - Page - Juz 29
﴿وَأَنَّ ٱلۡمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدۡعُواْ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدٗا ﴾
[الجِن: 18]
﴿وأن المساجد لله فلا تدعوا مع الله أحدا﴾ [الجِن: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kwa hakika misikiti ni ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, basi msiabudu humo asiyekuwa Yeye. Na mtakasieni maombi na ibada humo, kwani misikiti haikujengwa isipokuwa kwa ajili Mwenyezi Mungu Aabudiwe humo Peke Yake, na sio mwingine asiyekuwa Yeye. Katika haya kuna ulazima wa kuiepusha misikiti na kila kinachokoroga utakasaji wa Mwenyezi Mungu na ufuataji Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |