Quran with Swahili translation - Surah Al-Muzzammil ayat 19 - المُزمل - Page - Juz 29
﴿إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا ﴾
[المُزمل: 19]
﴿إن هذه تذكرة فمن شاء اتخذ إلى ربه سبيلا﴾ [المُزمل: 19]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika aya hizi zenye kutisha ambazo ndani yake kuna vigongaji na vikemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea |