×

Kama mnataka hukumu basi hukumu imekwisha kujieni. Na mkiacha itakuwa ndio kheri 8:19 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Anfal ⮕ (8:19) ayat 19 in Swahili

8:19 Surah Al-Anfal ayat 19 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 19 - الأنفَال - Page - Juz 9

﴿إِن تَسۡتَفۡتِحُواْ فَقَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡفَتۡحُۖ وَإِن تَنتَهُواْ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَعُودُواْ نَعُدۡ وَلَن تُغۡنِيَ عَنكُمۡ فِئَتُكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَوۡ كَثُرَتۡ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[الأنفَال: 19]

Kama mnataka hukumu basi hukumu imekwisha kujieni. Na mkiacha itakuwa ndio kheri kwenu. Na mkirejea Sisi pia tutarejea. Na jeshi lenu halitakufaeni kitu, japo likiwa kubwa. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن تستفتحوا فقد جاءكم الفتح وإن تنتهوا فهو خير لكم وإن تعودوا, باللغة السواحيلية

﴿إن تستفتحوا فقد جاءكم الفتح وإن تنتهوا فهو خير لكم وإن تعودوا﴾ [الأنفَال: 19]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Muombapo, enyi makafiri, kwa Mwenyezi Mungu Ayalete mateso na adhabu Yake kwa wale wenye kupita mipaka na kudhulumu, basi Mwenyezi Mungu Ameshaitikia maombi yenu Alipowaletea mateso Yake yaliyokuwa ni adhabu kwenu na ni mazingatio kwa wacha-Mungu. Na iwapo mtakomeka, enyi makafiri, kumkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kumpiga vita Nabii Wake, rehema na amani zimshukiye, hilo ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu. Na mkirudi vitani na kumpiga vita Muhammad, rehema na amani zimshukiye, na kuwapiga vita wafuasi wake Waumini, basi tutarudia kuwashinda kama mlivyoshindwa Siku ya Badr. Na hautawafaa mkusanyiko wenu kitu chochote kama ambavyo haukuwafaa siku ya Badr, pamoja na wingi wa idadi yenu na zana zenu na uchache wa idadi ya waumini na zana zao. Na Mwenyezi Mungu yuko pamoja na Waumini kwa kuwasaidia na kuwapa ushindi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek