Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 38 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِن يَنتَهُواْ يُغۡفَرۡ لَهُم مَّا قَدۡ سَلَفَ وَإِن يَعُودُواْ فَقَدۡ مَضَتۡ سُنَّتُ ٱلۡأَوَّلِينَ ﴾
[الأنفَال: 38]
﴿قل للذين كفروا إن ينتهوا يغفر لهم ما قد سلف وإن يعودوا﴾ [الأنفَال: 38]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia wale waliokanusha upweke wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa Washirikina wa watu wako kwamba watakomeka na ukafiri na kumfanyia uadui Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na wakarudi kumuamini Mwenyezi Mungu Peke Yake na kutompiga vita Mtume na Waumini, Mwenyezi Mungu Atawasamehe madhambi yaliyopita, kwani Uislamu unafuta yaliyopita. Na watakaporudia washirikina hawa kukupiga vita baada ya tukio ambalo ulipata ushindi juu yao siku ya Badr, basi mwendo wa watu wa mwanzo umetangulia, nao ni kwamba wao wakikanusha na wakaendelea kwenye ukaidi wao, tutawaletea adhabu na mateso kwa haraka |