Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 37 - الأنفَال - Page - Juz 9
﴿لِيَمِيزَ ٱللَّهُ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ وَيَجۡعَلَ ٱلۡخَبِيثَ بَعۡضَهُۥ عَلَىٰ بَعۡضٖ فَيَرۡكُمَهُۥ جَمِيعٗا فَيَجۡعَلَهُۥ فِي جَهَنَّمَۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ ﴾
[الأنفَال: 37]
﴿ليميز الله الخبيث من الطيب ويجعل الخبيث بعضه على بعض فيركمه جميعا﴾ [الأنفَال: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Atawakusanya na Atawatweza hawa ambao walimkanusha Mola wao na wakatoa mali yao kuwazuia watu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuzuia njia Yake isifuatwe, ili Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Apate kukipambanua kichafu na kizuri, na ili Ayakusanye Mwenyezi Mungu mali ya haramu, yaliyotumiwa kuwazuia watu na dini ya Mwenyezi Mungu, Ayaweke baadhi yake juu ya mengine yawe yamekusanyikana na kupandana kisha Ayatie kwenye Moto wa Jahanamu. Makafiri hawa ndio wenye kupata hasara duniani na Akhera |