Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 60 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿وَأَعِدُّواْ لَهُم مَّا ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن قُوَّةٖ وَمِن رِّبَاطِ ٱلۡخَيۡلِ تُرۡهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمۡ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمۡ لَا تَعۡلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعۡلَمُهُمۡۚ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيۡءٖ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيۡكُمۡ وَأَنتُمۡ لَا تُظۡلَمُونَ ﴾
[الأنفَال: 60]
﴿وأعدوا لهم ما استطعتم من قوة ومن رباط الخيل ترهبون به عدو﴾ [الأنفَال: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Tayarisheni, enyi makundi ya Waislamu,ili kukabiliana na maadui wenu, chochote mkiwezacho cha wingi wa watu na zana, ili muingize, kwa hio, kicho katika nyoyo za maadui wa Mwenyezi mungu na maadui wenu wanaowavizia; na muwatishe wengine ambao uadui wao bado haujajitokeza kwenu hivi sasa, lakini Mwenyezi Mungu Anawajua na Anayajua yale ambayo wanayadhamiria. Na mali yoyote na vinginevyo mnavyovitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, vingi au vichache, Mwenyezi Mungu Atawapa badala yake duniani na Atawaekea thawabu zake mpaka Siku ya Kiyama; na nyinyi hamtapunguziwa malipo ya hayo chochote |