Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 108 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿لَا تَقُمۡ فِيهِ أَبَدٗاۚ لَّمَسۡجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقۡوَىٰ مِنۡ أَوَّلِ يَوۡمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِۚ فِيهِ رِجَالٞ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُطَّهِّرِينَ ﴾
[التوبَة: 108]
﴿لا تقم فيه أبدا لمسجد أسس على التقوى من أول يوم أحق﴾ [التوبَة: 108]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Usisimame, ewe Nabii, kuswali katika msikiti huo kabisa. Kwani msikiti uliojengwa kwa misingi ya uchamungu kuanzia siku ya mwanzo, nao ni msikiti wa Qubā’, unafaa zaidi kwa wewe kusimama humo kwa kuswali. Kwani katika msikiti huu kuna watu wanapenda kujisafisha na najisi na uchafu kwa maji, kama wanavyojisafisha kwa kujiepusha na mambo yanayopelekea kufanya mambo yaliyoharamishwa na kuomba msamaha kutokana na madhambi na maasia. Na Mwenyezi Mungu Anawapenda wenye kujisafisha.Na iwapo msikiti wa Qubā’ ulijengwa juu ya misingi ya uchaji-Mungu, basi Msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ni kama hivyo kwa njia ya ubora zaidi na ustahiki zaidi |