Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 107 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مَسۡجِدٗا ضِرَارٗا وَكُفۡرٗا وَتَفۡرِيقَۢا بَيۡنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَإِرۡصَادٗا لِّمَنۡ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبۡلُۚ وَلَيَحۡلِفُنَّ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّا ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَٱللَّهُ يَشۡهَدُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ﴾
[التوبَة: 107]
﴿والذين اتخذوا مسجدا ضرارا وكفرا وتفريقا بين المؤمنين وإرصادا لمن حارب الله﴾ [التوبَة: 107]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanafiki waliojenga msikiti, kwa kuwadhuru Waumini, kumkanusha Mwenyezi Mungu na kuwagawanya Waumini, ili waswali humo baadhi yao na wauache msikiti wa Qubā’ ambao Waislamu wanaswali ndani yake, ili Waislamu watafautiane na wagawanyike kwa hilo, na kwa ajili ya kumngojea yule aliyempiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kabla ya hapo, naye ni Abū ‘Āmir al-Rāhib aliyeasi, ili pawe ni mahali pa kuwafanyia vitimbi Waislamu. Na wataapa tena wataapa, wanafiki hawa, kwamba wao hawakukusudia kwa kuujenga isipokuwa kuwafanyia wema na kuwahurumia Waislamu na kuwapa nafasi wanyonge wasioweza kwenda msikiti wa Qubā’ .Na Mwenyezi Mungu Anashuhudia kwamba wao ni warongo katika yale wanayoyaapia. Msikiti huo ulivunjwa na ukatiwa moto |