Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 110 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿لَا يَزَالُ بُنۡيَٰنُهُمُ ٱلَّذِي بَنَوۡاْ رِيبَةٗ فِي قُلُوبِهِمۡ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ﴾
[التوبَة: 110]
﴿لا يزال بنيانهم الذي بنوا ريبة في قلوبهم إلا أن تقطع قلوبهم﴾ [التوبَة: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Haliachi kuendelea, lile jengo wanafiki walilolijenga liwe ni madhara kwa msikiti wa Qubā’, kuwa ni ishara ya shaka unafiki uliojikita ndani ya nyoyo zao, mpaka nyoyo zao zikatike-katike kwa wao kuuawa au kufa au kwa kujuta kwao upeo wa kujuta nakurejea kwao kwa Mola wao na kumuogopa Yeye upeo wa kuogopa.Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa shaka waliyonayo hawa wanafiki na yale waliyoyakusudia kwa jengo lao, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo ya viumbe Vyake |