Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 41 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿ٱنفِرُواْ خِفَافٗا وَثِقَالٗا وَجَٰهِدُواْ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ ﴾
[التوبَة: 41]
﴿انفروا خفافا وثقالا وجاهدوا بأموالكم وأنفسكم في سبيل الله ذلكم خير لكم﴾ [التوبَة: 41]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tokeni, enyi Waumini, kwenda kwenye jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, vijana kwa wazee, katika uzito na wepesi, vyovyote mtakavyokuwa, mtoe mali zenu katika njia ya Mwenyezi Mungu na mupigane kwa mikono yenu ili kulitangaza neno la Mwenyezi Mungu. Kutoka huko na kupigana huko ni bora kwenu katika hali zenu za sasa na za baadaye kuliko kuwa wazito, kuacha kutoa na kujikalisha nyuma. Basi iwpo nyinyi ni miongoni mwa walio na ujuzi wa ubora wa jihadi na thawabu zake mbele ya Mwenyezi Mungu, fanyeni mliyoamrishwa na muitikie mwito wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake |