Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 42 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿لَوۡ كَانَ عَرَضٗا قَرِيبٗا وَسَفَرٗا قَاصِدٗا لَّٱتَّبَعُوكَ وَلَٰكِنۢ بَعُدَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلشُّقَّةُۚ وَسَيَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ لَوِ ٱسۡتَطَعۡنَا لَخَرَجۡنَا مَعَكُمۡ يُهۡلِكُونَ أَنفُسَهُمۡ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ إِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ ﴾
[التوبَة: 42]
﴿لو كان عرضا قريبا وسفرا قاصدا لاتبعوك ولكن بعدت عليهم الشقة وسيحلفون﴾ [التوبَة: 42]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, uliotukuka utukufu Wake, Ameliumbua kundi la wanafiki waliomtaka ruhusa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, ya kusalia nyuma na kutoenda kwenye vita vya Tabūk, kwa kueleza kwamba lau kutoka kwao kulikuwa ni kwa kuandama ngawira ya karibu iliyo nyepesi kuipata, wangalikuandama. Lakini walipoitwa kwenda kupigana na Warumi pambizoni mwa miji ya Shām katika kipindi cha joto, walitiana uvivu na wakajiweka nyuma. Na watatoa nyudhuru za kusalia kwao nyuma na kuacha kutotoka wakiapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao hawaliwezi hilo; wanaziangamiza nafsi zao kwa urongo na unafiki, na hali kwamba Mwenyezi Mungu yuwajua kuwa wao ni warongo katika zile nyudhuru zao wanazozitoa |