Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 43 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿عَفَا ٱللَّهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمۡ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْ وَتَعۡلَمَ ٱلۡكَٰذِبِينَ ﴾
[التوبَة: 43]
﴿عفا الله عنك لم أذنت لهم حتى يتبين لك الذين صدقوا وتعلم﴾ [التوبَة: 43]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Amekusamehe, ewe Nabii, kwa yale yaliyotokea kwako, ya kuliacha lililo bora zaidi na la ukamilifu zaidi, nayo ni yale ya kuwaruhusu wanafiki kukaa wasiende kwenye jihadi. Ni kwa nini uwaruhusu hawa wakae wasiende vitani, usingojee mpaka wakufunukie waziwazi wale waliosema kweli katika kutaja nyudhuru zao na uwajue warongo miongoni mwao katika hilo |