Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 72 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّٰتِ عَدۡنٖۚ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ أَكۡبَرُۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ﴾
[التوبَة: 72]
﴿وعد الله المؤمنين والمؤمنات جنات تجري من تحتها الأنهار خالدين فيها ومساكن﴾ [التوبَة: 72]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Amewaahidi wenye kumuaumini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, waume na wake, mabustani ya Pepo ambayo chini yake inapita mito, hali ya kukaa humo milele. Starehe zake haziwaondokei. yana majumba yaliojengwa vizuri yenye utulivu mzuri katika mabustani ya makao. Na radhi itokayo kwa Mwenyezi Mungu watakayoipata ni kubwa zaidi na ni bora zaidi kuliko starehe walizonazo. Ahadi hiyo ya malipo mema ya Akhera ndio kufaulu kukubwa |