Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 91 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[التوبَة: 91]
﴿ليس على الضعفاء ولا على المرضى ولا على الذين لا يجدون ما﴾ [التوبَة: 91]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watu wenye nyudhuru, miongoni mwa madhaifu, wagonjwa na mafukara ambao hawamiliki mali ya kuwawezesha kufanya matayarisho ya kutoka, hawana makosa ya kujikalia, iwapo wamemtakasia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wameifuata sheria Yake kivitendo. Hapana njia yoyote kwa wale waliozuiliwa na udhuru kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kupatiwa mateso na kutiwa makosani, iwapo wao ni waaminifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa watenda wema (muhsinūn), ni Mwenye kuwarehemu |