Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 90 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَجَآءَ ٱلۡمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ لِيُؤۡذَنَ لَهُمۡ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[التوبَة: 90]
﴿وجاء المعذرون من الأعراب ليؤذن لهم وقعد الذين كذبوا الله ورسوله سيصيب﴾ [التوبَة: 90]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kilikuja kikundi, miongoni mwa watu wa vitongoji vya Waarabu wa majangwani, kandokando ya mji wa Madina wakitoa nyudhuru kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, wakimuelezea udhaifu walionao na kutoweza kwao kutoka kwenda vitani. Na kuna watu waliojikalia bila kutoa udhuru wowote kwa kumfanyia ujasiri Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema wa Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Basi wale waliokufuru miongoni mwa hawa itawatapata adhabu kali, ya kuuawa na nyinginezo hapa duniani, na ya Moto kesho Akhera |