Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 101 - يُونس - Page - Juz 11
﴿قُلِ ٱنظُرُواْ مَاذَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَا تُغۡنِي ٱلۡأٓيَٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوۡمٖ لَّا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[يُونس: 101]
﴿قل انظروا ماذا في السموات والأرض وما تغني الآيات والنذر عن قوم﴾ [يُونس: 101]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wako, «Fikirini na mzingatie kwa yaliyomo mbinguni na ardhini miongoni mwa aya za Mwenyezi Mungu zilizo waziwazi.» Lakini aya, mazingatio na Mitume wenye kuwaonya waja wa Mwenyezi Mungu adhabu Yake, vyote hivyo havikuwa ni vyenye kuwanufaisha watu wasioamini chochote katika hivyo, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na ujeuri wao |