Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 107 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَإِن يَمۡسَسۡكَ ٱللَّهُ بِضُرّٖ فَلَا كَاشِفَ لَهُۥٓ إِلَّا هُوَۖ وَإِن يُرِدۡكَ بِخَيۡرٖ فَلَا رَآدَّ لِفَضۡلِهِۦۚ يُصِيبُ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ ﴾
[يُونس: 107]
﴿وإن يمسسك الله بضر فلا كاشف له إلا هو وإن يردك بخير﴾ [يُونس: 107]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Akikupatia, ewe Mtume, shida au mitihani, basi hakuna wa kuyaondoa hayo isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, na Akikutakia furaha na neema, basi hakuna yoyote mwenye kuyazuia hayo. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Anampatia furaha na shida Anayemtaka kati ya waja Wake. Na Yeye ni Mwingi wa msamaha wa dhambi za wenye kutubia, ni Mwingi wa rehema kwa wanaomuamini na kumtii |