Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 106 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَلَا تَدۡعُ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَۖ فَإِن فَعَلۡتَ فَإِنَّكَ إِذٗا مِّنَ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[يُونس: 106]
﴿ولا تدع من دون الله ما لا ينفعك ولا يضرك فإن فعلت﴾ [يُونس: 106]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala usiwaombe, ewe Mtume, wasiokuwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa mizimu na masanamu, kwani wao hawanufaishi wala hawadhuru. Na ufanyapo hilo na ukawaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu, hapo wewe utakuwa ni miongoni mwa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wenye kujidhulumu nafsi zao kwa ushirikina na kufanya maasia. Maneno haya ingawa anaambiwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, pia wanaambiwa umma wote |