×

Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni 10:31 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Yunus ⮕ (10:31) ayat 31 in Swahili

10:31 Surah Yunus ayat 31 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 31 - يُونس - Page - Juz 11

﴿قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أَمَّن يَمۡلِكُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَمَن يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُۚ فَقُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ ﴾
[يُونس: 31]

Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri mambo yote? Watasema: Allah, Mwenyezi Mungu. Basi sema: Je! Hamchi

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل من يرزقكم من السماء والأرض أمن يملك السمع والأبصار ومن يخرج, باللغة السواحيلية

﴿قل من يرزقكم من السماء والأرض أمن يملك السمع والأبصار ومن يخرج﴾ [يُونس: 31]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa, «Ni nani anayewaruzuku kutoka juu kwa mvua anayoiteremsha, na kutoka ardhini kwa mimea na miti aina mbalimabali anayoiotesha kutoka humo, ambayo miongoni mwayo mnakula nyinyi na wanyama wenu? Na ni nani anayemiliki hisia za kusikia na za kuona mnazostarehea, nyinyi na wengineo? Na ni nani anayemiliki uhai na kifo, katika ulimwengu wote, akawatoa wenye uhai na wafu, baadhi yao kutoka kwa wengine, katika viumbe mnavyovijua na msivyovijua? Na ni nani anayeyaendesha mambo ya mbinguni na ardhini na yaliyomo ndani yake, (anayeyaendesha) mambo yenu nyinyi na mambo ya viumbe vyote?» Watakujibu kwamba anayefanya yote hayo ni Mwenyezi Mungu. Waambie, «Basi si muogope mateso ya Mwenyezi Mungu mnapomuabudu mwingine pamoja na Yeye?»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek