Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 110 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ ﴾
[هُود: 110]
﴿ولقد آتينا موسى الكتاب فاختلف فيه ولولا كلمة سبقت من ربك لقضي﴾ [هُود: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hakika tulimpa Mūsā Kitabu , nacho ni Taurati, wakatafautiana watu wake juu yake: baadhi yao walikiamini na wengine walikikanusha, kama walivyofanya watu wako kuhusu Qur'ani. Na lao si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kutowaharakishia adhabu viumbe Wake, ingaliwashukia wao duniani kwao hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwaangamiza wenye kukanusha na kuwaokoa Waumini. Na makafiri wa watu wako, miongoni mwa mayahudi na washirikina, ewe Mtume, wako kwenye shaka inayowatia wasiwasi juu hii Qur'ani |