Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 27 - هُود - Page - Juz 12
﴿فَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا نَرَىٰكَ إِلَّا بَشَرٗا مِّثۡلَنَا وَمَا نَرَىٰكَ ٱتَّبَعَكَ إِلَّا ٱلَّذِينَ هُمۡ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ ٱلرَّأۡيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلِۭ بَلۡ نَظُنُّكُمۡ كَٰذِبِينَ ﴾
[هُود: 27]
﴿فقال الملأ الذين كفروا من قومه ما نراك إلا بشرا مثلنا وما﴾ [هُود: 27]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakasema wakubwa wa ukafiri miongoni mwa watu wake, «Wewe si Malaika bali wewe ni binadamu, inakuwaje wewe uletewe wahyi bila sisi? Na hatukuoni umefuatwa isipokuwa na watwevu wetu, na wao wamekufuata bila kufikiria wala kupima. Na sisi hatuwaoni nyinyi kuwa muna ubora wowote juu yetu, wa riziki wala mali, tangu mlipoingia kwenye dini yenu hii. Bali sisi tunaamini kwamba nyinyi ni warongo katika madai yenu |