Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 78 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَجَآءَهُۥ قَوۡمُهُۥ يُهۡرَعُونَ إِلَيۡهِ وَمِن قَبۡلُ كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطۡهَرُ لَكُمۡۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُخۡزُونِ فِي ضَيۡفِيٓۖ أَلَيۡسَ مِنكُمۡ رَجُلٞ رَّشِيدٞ ﴾
[هُود: 78]
﴿وجاءه قومه يهرعون إليه ومن قبل كانوا يعملون السيئات قال ياقوم هؤلاء﴾ [هُود: 78]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watu wa Lūṭ wakamjia kwa haraka kutaka kufanya uchafu, na kabla ya kuja kwao walikuwa wanawendea wanaume kwa njia ya matamanio badala ya wanawake. Lūṭ akasema kuwaambia watu wake, «Hawa ni watoto wangu wa kike, waoeni. Wao niwasafi zaidi kwenu kuliko hayo mnayoyataka.» Aliwaita kuwa ni watoto wake wa kike sababu Nabii wa umma ana daraja ya baba kwao. «Basi muogopeni Mwenyezi Mungu na mjihadhari na mateso Yake, wala msinifedhehi kwa kuwakosea wageni wangu. Kwani hakuna mtu yoyote katika nyinyi aliye mzuri wa kupima mambo apate kuwakataza wanaotaka kufanya machafu akawzuia wao na hayo? Kumdhalilisha mgeni ni jambo la kutukanisha hakuna alifanyalo isipokuwa ni watu wa utwevu.» |