Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 50 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿وَقَالَ ٱلۡمَلِكُ ٱئۡتُونِي بِهِۦۖ فَلَمَّا جَآءَهُ ٱلرَّسُولُ قَالَ ٱرۡجِعۡ إِلَىٰ رَبِّكَ فَسۡـَٔلۡهُ مَا بَالُ ٱلنِّسۡوَةِ ٱلَّٰتِي قَطَّعۡنَ أَيۡدِيَهُنَّۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيۡدِهِنَّ عَلِيمٞ ﴾
[يُوسُف: 50]
﴿وقال الملك ائتوني به فلما جاءه الرسول قال ارجع إلى ربك فاسأله﴾ [يُوسُف: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mfalme akasema kuwaambia wasaidizi wake, «Mtoeni jela huyo mtu aliyeagua ndoto, na mleteni kwangu.» Yule aliyetumwa na mfalme alipomjia (Yūsuf) kumwita. Yūsuf alisema kumwambia, «Rudi kwa bwanako mfalme umtake awaulize wanawake walioijaruhi mikono yao juu ya uhakika wa mambo yao na habari zao na mimi, ili ukweli ufunuke kwa wote, na kutokuwa na hatia kwangu kuwe wazi, kwani Mola wangu ni Mjuzi zaidi wa mambo waliyoyapanga na waliyoyafanya, hakuna chochote kinachofichika Kwake katika hayo.» |