Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 51 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿قَالَ مَا خَطۡبُكُنَّ إِذۡ رَٰوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفۡسِهِۦۚ قُلۡنَ حَٰشَ لِلَّهِ مَا عَلِمۡنَا عَلَيۡهِ مِن سُوٓءٖۚ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡـَٰٔنَ حَصۡحَصَ ٱلۡحَقُّ أَنَا۠ رَٰوَدتُّهُۥ عَن نَّفۡسِهِۦ وَإِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ ﴾
[يُوسُف: 51]
﴿قال ما خطبكن إذ راودتن يوسف عن نفسه قلن حاش لله ما﴾ [يُوسُف: 51]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mfalme akasema kuwaambia wanawake walioijaruhi mikono yao. «Habari zenu ni zipi, mlipomtaka Yūsuf siku ya makaribisho? Kwani mliona chochote kutoka kwake chenye kutia shaka?» Wakasema, «Mwenyezi Mungu Atulinde! Hatujui chochote hata kidogo cha kumtia ila.» Hapo alisema mke wa Kiongozi, «Sasa umefunuka ukweli baada ya kufichika. Mimi ndiye niliyejaribu kumtia hatiani kwa kumbembeleza, na akakataa. Na yeye ni katika wakweli katika kila alilolisema |