Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 76 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿فَبَدَأَ بِأَوۡعِيَتِهِمۡ قَبۡلَ وِعَآءِ أَخِيهِ ثُمَّ ٱسۡتَخۡرَجَهَا مِن وِعَآءِ أَخِيهِۚ كَذَٰلِكَ كِدۡنَا لِيُوسُفَۖ مَا كَانَ لِيَأۡخُذَ أَخَاهُ فِي دِينِ ٱلۡمَلِكِ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ وَفَوۡقَ كُلِّ ذِي عِلۡمٍ عَلِيمٞ ﴾
[يُوسُف: 76]
﴿فبدأ بأوعيتهم قبل وعاء أخيه ثم استخرجها من وعاء أخيه كذلك كدنا﴾ [يُوسُف: 76]
Abdullah Muhammad Abu Bakr wakarudi na ndugu zake Yūsuf kwake, akasimama mwenyewe kupekua mizigo yao. Akaanza na mizigo yao kabla ya mzigo wa ndugu yake, ili kuimarisha mpango wake wa kumfanya ndugu yake abakie pamoja na yeye, kisha akamalizikia kwenye vyombo vya ndugu yake na akakitoa chombo humo. Hivyo ndivyo tulivyomsahilishia Yūsuf mpango huu ambao ulimpelekea kumchukua ndugu yake kwenye mamlaka ya mfalme wa Misri. Kwani si katika dini yake kummiliki mwizi, isipokuwa kwamba matakwa ya Mwenyezi Mungu yamepelekea mipango hii na kutaka uamuzi kwenye sheria ya ndugu zake Yūsuf yenye hukumu ya mwizi kufanywa mtumwa. Tunawainua daraja tunaowataka ulimwenguni juu ya mwingine kama vile tulivyomuinua Yūsuf daraja. Na juu ya kila mwenye ujuzi kuna mjuzi zaidi kuliko yeye, mpaka ujuzi ukome kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Mjuzi wa yaliyofichika na yanayoonekana |