Quran with Swahili translation - Surah Ar-Ra‘d ayat 18 - الرَّعد - Page - Juz 13
﴿لِلَّذِينَ ٱسۡتَجَابُواْ لِرَبِّهِمُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَٱلَّذِينَ لَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُۥ لَوۡ أَنَّ لَهُم مَّا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ سُوٓءُ ٱلۡحِسَابِ وَمَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ ﴾
[الرَّعد: 18]
﴿للذين استجابوا لربهم الحسنى والذين لم يستجيبوا له لو أن لهم ما﴾ [الرَّعد: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Pepo ni ya wenye kuamini ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na Moto ni wa wale ambao hawakumtii na wakamkanusha. Na lau walikuwa wanamiliki kila kilichoko ardhini na zaidi ya kama hiko pamoja nacho, wangalikitoa kwa kujikomboa nafsi zao na adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama, na hakingalikubaliwa kutoka kwao. Wao watafanyiwa hesabu kwa kila tendo baya walilolitenda. Na makazi yao ya kukaa ni Jahanamu, itakuwa ni tandiko kwao. Na tandiko baya mno ni hilo walilojitayarishia nafsi zao |