Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 18 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿مَّثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَرَمَادٍ ٱشۡتَدَّتۡ بِهِ ٱلرِّيحُ فِي يَوۡمٍ عَاصِفٖۖ لَّا يَقۡدِرُونَ مِمَّا كَسَبُواْ عَلَىٰ شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلۡبَعِيدُ ﴾
[إبراهِيم: 18]
﴿مثل الذين كفروا بربهم أعمالهم كرماد اشتدت به الريح في يوم عاصف﴾ [إبراهِيم: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hali ya matendo mazuri ya makafiri ulimwenguni, kama vile kufanya wema na kuunga zao, ni kama hali ya jivu lililopigwa na upepo wa nguvu katika siku yenye upepo mkali usiache hata alama yake. Hivyo ndivyo yatakavyokuwa matendo yao, hawatapata kwa matendo hayo kitu cha kuwanufaisha mbele ya Mwenyezi Mungu; kwani ukafiri umeyaondoa kama vile upepo ulivyoondoa jivu. Kushughulika huko na kufanya matendo mema huko bila ya msingi, ndio kupotea kuliko mbali na njia ya sawa |