Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 25 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿تُؤۡتِيٓ أُكُلَهَا كُلَّ حِينِۭ بِإِذۡنِ رَبِّهَاۗ وَيَضۡرِبُ ٱللَّهُ ٱلۡأَمۡثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ ﴾
[إبراهِيم: 25]
﴿تؤتي أكلها كل حين بإذن ربها ويضرب الله الأمثال للناس لعلهم يتذكرون﴾ [إبراهِيم: 25]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Unatoa matunda yake kila kipindi kwa idhini ya Mola wake. Namna hiyo ndivyo ulivyo mti wa Imani: msingi wake umejikita imara ndani ya moyo wa Muumini kiujuzi na kiitikadi, na tagaa zake za matendo mema na tabia za kuridhisha zinapaishwa juu kwa Mwenyezi Mungu, na malipo yake mema yanapatikana kila kipindi. Na Mwenyezi Mungu Anawapigia watu mfano ili wakumbuke na wawaidhike wapate kuzingatia |