Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 26 - إبراهِيم - Page - Juz 13
﴿وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٖ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ ٱجۡتُثَّتۡ مِن فَوۡقِ ٱلۡأَرۡضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٖ ﴾
[إبراهِيم: 26]
﴿ومثل كلمة خبيثة كشجرة خبيثة اجتثت من فوق الأرض ما لها من﴾ [إبراهِيم: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na mfano wa neno ovu, nalo ni neno la ukafiri, ni kama mti muovu wa chakula na ladha, nao ni mti wa subili, uliong’olewa juu ya ardhi, kwa kuwa mizizi yake iko karibu na uso wa ardhi, hauna mizizi iliyojikita ndani wala hauna tagaa zenye kwenda juu. Hivo ndivyo kafiri alivyo, hana uthabiti wala hana wema na wala hakuna tendo lema lake lolote litakalopaishwa kwa Mwenyezi Mungu |