×

Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha 14:27 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Ibrahim ⮕ (14:27) ayat 27 in Swahili

14:27 Surah Ibrahim ayat 27 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Ibrahim ayat 27 - إبراهِيم - Page - Juz 13

﴿يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱلۡقَوۡلِ ٱلثَّابِتِ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّٰلِمِينَۚ وَيَفۡعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ ﴾
[إبراهِيم: 27]

Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: يثبت الله الذين آمنوا بالقول الثابت في الحياة الدنيا وفي الآخرة ويضل, باللغة السواحيلية

﴿يثبت الله الذين آمنوا بالقول الثابت في الحياة الدنيا وفي الآخرة ويضل﴾ [إبراهِيم: 27]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Anawathibitisha wale waloamini kwenye neno la ukweli lenye uimara nalo ni kukubali kwamba hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhaamad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwamba Atawathibitisha kwenye dini ya kweli aliyokuja nayo katika huu ulimwengu, Atawapa mwisho mwema wakati wa kufa, na Atawaongoza watoe jawabu ya sawa watakapoulizwa na Malaika wawili kaburini. Na Mwenyezi Mungu Atawapoteza madhalimu wasiuone usawa ulimenguni na Akhera. Na Mwenyezi Mungu Anafanya Analolitaka kwa kuwaafikia wenye kuamini na kutowaongoza wenye kukufuru na kuasi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek