Quran with Swahili translation - Surah An-Nahl ayat 49 - النَّحل - Page - Juz 14
﴿وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ ﴾
[النَّحل: 49]
﴿ولله يسجد ما في السموات وما في الأرض من دابة والملائكة وهم﴾ [النَّحل: 49]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu Peke Yake vyote vilivyo mbinguni na vilivyo ardhini, miongoni mwa vinavyotambaa. Na Malaika wanamsujudia Mwenyezi Mungu, na wao hawafanyi ujeuri kwa kukataa kumuabudu Yeye. Na Amewahusu Malaika kwa kuwataja baada ya kuwakusanya pamoja na viumbe wengine, kutokana na utukufu wao, ubora wao na wingi wa kuabudu kwao |