Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 16 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَإِذَآ أَرَدۡنَآ أَن نُّهۡلِكَ قَرۡيَةً أَمَرۡنَا مُتۡرَفِيهَا فَفَسَقُواْ فِيهَا فَحَقَّ عَلَيۡهَا ٱلۡقَوۡلُ فَدَمَّرۡنَٰهَا تَدۡمِيرٗا ﴾
[الإسرَاء: 16]
﴿وإذا أردنا أن نهلك قرية أمرنا مترفيها ففسقوا فيها فحق عليها القول﴾ [الإسرَاء: 16]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tukitaka kuwaangamiza watu wa mji kwa udhalimu wao, tunawaamrisha wenye gogi wao wamtii Mwenyezi Mungu, wampwekeshe na wawaamini Mitume Wake, na wasokuwa wao wako nyuma yao kwa kuwafuata, wakaasi amri ya Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake, hapo likapasa juu yao neno la adhabu ambalo hakuna namna ya kurudishwa, na tukawamaliza kwa maangamivu yaliyotimia |