Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 47 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَسۡتَمِعُونَ بِهِۦٓ إِذۡ يَسۡتَمِعُونَ إِلَيۡكَ وَإِذۡ هُمۡ نَجۡوَىٰٓ إِذۡ يَقُولُ ٱلظَّٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلٗا مَّسۡحُورًا ﴾
[الإسرَاء: 47]
﴿نحن أعلم بما يستمعون به إذ يستمعون إليك وإذ هم نجوى إذ﴾ [الإسرَاء: 47]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi tunayajua zaidi yale wanayoyasikiliza viongozi wa Kikureshi pale wakusikilizapo na hali nia zao ni mbovu. Kusikiliza kwao si kwa ajili ya kutaka kuogoka na kuikubali haki. Na sisi tunajua kule kunong’onezana kwao wanaposema, «Hamumfuati isipopkuwa ni mwanamume aliyerogwa na akili yake ikabadilika.» |