Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 79 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَتَهَجَّدۡ بِهِۦ نَافِلَةٗ لَّكَ عَسَىٰٓ أَن يَبۡعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامٗا مَّحۡمُودٗا ﴾
[الإسرَاء: 79]
﴿ومن الليل فتهجد به نافلة لك عسى أن يبعثك ربك مقاما محمودا﴾ [الإسرَاء: 79]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na inuka, ewe Nabii, kutoka kwenye usingizi sehemu ya usiku, usome Qur’ani katika Swala ya usiku, ipate kuwa, hiyo Swala ya usiku, ni nyongeza kwako katika utukufu wa cheo na kupandishiwa daraja. Huenda Mwenyezi Mungu Akakuleta uwe ni mwenye kuwashufaia watu Siku ya Kiyama, ili Mwenyezi Mungu Awarehemu kwa kuwaondolea waliokuwa nayo, na usimame kisimamo ambacho watakushukuru kwacho wa mwanzo na wa mwisho |