Quran with Swahili translation - Surah Al-Kahf ayat 37 - الكَهف - Page - Juz 15
﴿قَالَ لَهُۥ صَاحِبُهُۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَكَفَرۡتَ بِٱلَّذِي خَلَقَكَ مِن تُرَابٖ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٖ ثُمَّ سَوَّىٰكَ رَجُلٗا ﴾
[الكَهف: 37]
﴿قال له صاحبه وهو يحاوره أكفرت بالذي خلقك من تراب ثم من﴾ [الكَهف: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenzake Muumini akamwambia, huku akimjadili kwa kumuwaidhia, «Vipi wewe utamkanusha Mwenyezi Mungu Aliyekuumba kwa mchanga kisha kwa tone la manii kisha Akakusawazisha kwa kukufanya binadamu mwenye kimo kilicholingana na umbo?» Katika aya hii pana dalili ya kwamba mwenye uweza wa kuanzisha kuumba viumbe ni muweza wa kuwarudisha |